Makundi ya Kombe la Dunia 2018
Shirika la soka ulimwenguni (FIFA) limetangaza makundi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Urusi.
Katika makundi hayo makundi yanayoonekana hatari zaidi ni Kundi C ambako kuna Ufaransa, Australia, Peru na Denmark na Kundi F linaloundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya watu Korea.
Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika kati ya Mwenyeji, Urusi dhidi ya Saudi Arabia tarehe 14 juni 2018 kunako dimba la Luzhniki.
No comments:
Post a Comment