Muingizaji wa filamu nchini,Jacklyn Wolper amesema pamoja na kuwa na
mahusiano na wasanii wenzake akiwemo Diamond,Jux. lakini Ally Kiba ndiye
msanii pekee aliyemtambulisha kwenye ulimwengu mtamu wa mapenzi.
Akiongea na Global Publishers,muingizaji huyo alisema aliachana na Ally
Kiba kwasababu ya wanawake wengi walikuwa wakimtamani kimapenzi.
“Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka.
Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya
utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza
kwenye ulimwengu wa mapenzi'Alisema Wolper
“Ali akawa
staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi
sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na
tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.”alisema Wolper
Vipi kuhusu Jux?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule
mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu
nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa
sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,”alisema.
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa
kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini
tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi
tena kama zamani,” alisema Wolper.
Bongo Forest
Alikiba
Bongo movie
Diamond
Wolper: Alikiba alinifundisha mapenzi, Diamond alikuwa halali bila kuniona ila nilimpenda sana Jux

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment