Breaking News
recent

Future kutumbuiza kwenye MTV MAMA pamoja na Diamond na Alikiba

Rapper wa Marekani, Future, ametangazwa kuwa msanii wa nje ya Afrika atakayetumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22.
Future ataungana na Alikiba na Diamond na wasanii wengine wa Afrika kwenye orodha ya wale watakaotumbuiza jioni hiyo jijini Johannesburg.
“We are proud to announce that @1future will be joining for the #MTVMAMA2016!!! #FutureMTVMAMA,” wameandika MTV Base kwenye Twitter.
Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Nayvadius DeMun Wilburn ana album nne hadi sasa, Pluto (2012), Honest (2014), DS2 (2015) na EVOL (2016).
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.