Waziri
mkuu Mizengo Pinda amesema serikali imeagiza kuzingatiwa sheria ya vifo
vyenye utata kwa kufanyika uchunguzi wa kina juu ya vifo hivyo ambapo
pia amekanusha stori kwamba Tanzania imechafuka kwenye anga za kimataifa
kutokana na matukio mbalimbali yaliyotokea.
Hii
ni stori kutoka 104.4 Dodoma bungeni wakati akijibu swali la kiongozi
wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo
ambapo ameamlfy kwamba kuwepo kwa hisia kuwa serikali inahusika
katika
mauaji ya raia sio sahihi na hata ishu ya Kiongozi wa Madaktari Dr
Ulimboka Steven kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika sio vizuri
ikatumiwa kama mfano.
Freeman
Mbowe alimuuliza waziri mkuu kwamba “Mheshimiwa Waziri mkuu katika nchi
yetu kwa muda mrefu sasa yamekuwepo mauaji mengi na baadhi ya vifo hivi
vimekua na utata mkubwa na baadhi ya vifo hivi vimekua vikihisiwa
kuhusisha vyombo vya dola kama vile jeshi la Polisi, lakini ni kweli
kwamba hisia za dola kuhusika katika mateso na mauaji ya raia
zimeendelea kuwepo na jinsi ninavyouliza swali hili sifa ya taifa letu
iko mashakani katika anga za kimataifa kutokana na mateso ambayo
yanaonekana yalikua na kusudio la mauaji ambayo alifanyiwa mwenyekiti wa
madaktari Dr Steven Ulimboka”Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “Sio kweli kwamba jina la nchi yetu limechafuka, kuchafuka sana kwa lipi? ukisema hivyo ni lazima vilevile uwepo ushahidi wa dhati unaoonyesha kwamba ni kweli serikali inahusika, sasa umetumia mfano wa Ulimboka… sio mfano mzuri, we huna ushahidi kama ni serikali imefanya hivyo na hakuna mpaka sasa anaeweza kusema ana ushahidi huo, ndio maana tulisema mara ya mwisho kwamba ni vizuri jambo hili likafanyiwa uchunguzi wa kina ili tujue
kilichotokea hasa ni kitu gani”
Kwa
kumalizia kumjibu Freeman Mbowe, Waziri mkuu amesema “hainiingii
kichwani hata kidogo kwa mtu ambae tumekua tunafanya nae kazi muda wote
alafu sisi hao hao tuchukue hatua tena ya kutaka kwenda kumuadhibu kwa
namna iliyotokea, haiingii kichwani”
Kwenye
sentensi nyingine ni kwamba Waziri Mkuu amesema serikali imefanya
jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa kwenye
hospitali ya Taifa Muhimbili ambako hivi karibuni taasisi ya moyo
itazinduliwa, ameamplfy pia kwamba hatua nyingine ni kuipandisha hadhi
hospitali ya Jeshi Lugalo ili kuwa hospitali ya rufaa.
No comments:
Post a Comment