-Yanatoka nchi jirani, yanatengenezwa kwa umeme
Ripoti ya Wiki hii imegundua kuwa asilimia kubwa ya mayai yanayotumiwa
na wananchi wengi kwa sasa ni feki na yanauzwa kinyemela ndani ya Jiji
la Dar.
Baada ya kupigwa vita na serikali miezi michache iliyopita, imebainika
kuwa bado yamezagaa na watu wanaotajwa kuyatumia kwa kiasi kikubwa ni
wauza chipsi mitaani.
Mayai hayo ambayo hayatofautiani na mayai ya
kuku wa kizungu yaliyozoeleka kwa kuwa na muonekano wa rangi nyeupe
sana, imebainika kuwa yanatengenezwa kwa kutumia mashine maalum za
umeme.
Ili kubaini uwepo wa mayai hayo ambayo serikali kupitia Bodi
ya Chakula na Dawa (TFDA), iliwatahadharisha wananchi kutotumia kwa
madai kuwa yana madhara kiafya, cha kushangaza bado yamezagaa mitaani
kama njugu.
Ripoti ya Wiki imejaribu kufanya utafiti wa kina na
kugundua uwepo wa mayai hayo hasa katika maeneo ya Buguruni na Sinza,
Dar ambapo ilidaiwa kuwa mzigo mkubwa wa mayai hayo ulitokea nchini
Kenya.
Aidha, kuanza kuuzwa tena kwa mayai hayo siku za hivi
karibuni, kunatokana na wakazi wa jiji kutojali aina ya vyakula
wanavyokula, jambo linalotoa mwanya kwa wachuuzi hao kuyapenyeza mayai
hayo kwa siri kwenye mzunguko wa mayai ya kawaida.
Ripoti ya Wiki
ilizungumza na mmoja wa wauza chipsi waliokutwa na mayai hayo ambaye
alikiri uwepo wa mayai hayo na kubainisha kuwa yanasambazwa na wauzaji
wakubwa ambao wanasemekana kuwa waliyanunua kwa wingi kabla serikali
haijayapiga marufuku.
“Haya mayai mbona yapo mengi tu. Sinza nzima,
ukiuliza unayapata. Watu wengi wanayakataa. Ambao hawayajui
tunawabambikizia wanakula,” alisema muuza chipsi huyo kwa sharti la
kutotajwa jina.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment