Mtayarishaji wa muziki anayetamba kwa sasa,Nahreel kutokea studio ya
The Industry amesema kuwa mwaka 2015 ndio umekuwa wa neema kwake kwani
ndio mwaka ambao pochi lake limetuna sana kwa kutengeneza mkwanja mrefu
zaidi kwenye tasnia hiyo kuliko miaka mingine yote huku akitingisha
mawimbi ya redio kwa hits zaidi ya 16 kutokea mikononi mwake.
Nahreel amesema kuwa mwaka jana ameweza kupata nafasi ya kushiriki
kwenye coke studio nchini kenya ambapo alikatiwa mkwanja unaovutia pia
ukitoa kazi za studio ameweza kupata deals za matangazo nyingi.
“kweli,muziki unalipa na mimi kama
producer umenilipa kwa njia nyingi,kwa wasanii kunilipa studio,kwa kazi
nazopata off studio.Mwaka 2015 nilihusika kwenye coke studio nililipwa
hela nzuri,nilipata radio adverts za makampuni tofauti..as producer
nimenufaika sana mwaka 2015 kuliko miaka mingine yote“alifunguka producer huyo ambaye pia ni msanii wa navy Kenzo.
Bongo Forest
Navy Kenzo
Producer Nahreel ameingiza Pesa zaidi mwaka 2015,ametengeneza hits zaidi ya 16

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment