Mwanadada Saraha Kaisi aka Shaa anayetamba na ngoma yake ‘Sugua Gaga’ni
ngoma iliyompa chati kubwa kwa mashabiki wake wa ndani na nje ya Bongo.
Shaa baada ya kuona amepata mafanikio makubwa kutokana na ngoma yake
hiyo ikambidi aongeze mkataba wa mwaka mmoja baada ya mkataba wa miezi
sita kuisha na Mkurugenzi wa TMK Family na Mkubwa na Wanawe Said Fella.
Mwanadada huyo alizungumza kupitia swali lililoulizwa na host wa
kipindi cha Clouds E Shadee nakusema “Nimeongeza mkataba na Mkubwa Na
Wanae ambao awali ulikuwa wa miezi sita sasa nimeongeza miezi sita tena
na umekuwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kugundua kuwa ngoma ya Sugua
Gaga niliyoifanya imeshika chati sana, ata hivyo natarajia kufanya ngoma
kali zaidi ya Sugua Gaga.” alisema Shaa.
Hata hivyo mwanadada huyo hakueleza wazi kama ni lini wanaanza mchakato wakuifanya ngoma yake mpya.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment