Breaking News
recent

Producer Pancho Latino aeleza sababu ya kujichora tatoo ya jina la Dully Sykies


Producer  Pancho Latino alifanya kazi kwa mara kwanza kama producer kwenye studio za Dhahabu records ya Dully Sykies  na kutengeneza ngoma kali kama Dar es salaam stand up ya Chidy Benz na nyingine nyingi. Akiongea na mohamedjaku.blogspot.com,mpishi Pancho kama Chidy Benz alivyomuita kwenye mistari ya Dar es salaam stand up alisema,

”Dully kwenye muziki ni baba yangu, kama mtoto anavyoanza kukua nyumbani. Basi na mimi nikua kwenye muziki kwenye studio ya Dully Dhahabu records. Aliweza kuniamini na kunipa nafasi kwenye studio yake na nikafanya kazi na wasanii wengi wakubwa. Pale ndiyo nilipopitia hadi kufika hapa nilipofika leo. Heshima yake ni kubwa sana na niliitaji kuweka kumbukumbu kwa hilo, so tatoo ni njia nzuri sana ”

Oky, so kitu kingine mtu wangu wa nguvu unaweza kujiuliza hii tatoo ni moja kwa moja au ni ya muda tu?.Pancho Latino anaendelea kuelezea,”Nisingeweza kuweka tatoo ya muda kwa jina la Dully Sykies. Tangu nina miaka 18 nipo chini yake nakua kwenye muziki, anastahili kumbukumbu ya moja kwa moja. So hii tatoo sio ya muda, ipo hapa permanent”.
 
Yaliyoendelea kwenye comment za Instagram

Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.