Msanii ambaye anaunda kundi la TMK wanaume family maarufu kama Chege
au mwenyewe hupenda kujiita Chege Chigunda mtoto wa mama Saidi, aliwahi
kujihusisha na biashara nyingine ya kuuza nguo kwenye duka lake la
Chigunda Classic. Duka la Chigunda Classic lilikuwa maeneo ya Kinondoni ndani yake kulikuwa na nguo tofauti. Baada ya kufanya biashara hiyo
kwa muda kadhaa, Chege aliamua kulifunga. Baada ya hapo alifungua
barbershop ambayo likuwa mitaa ya Kinondoni hapo hapo pia. Lakini muda
ulifika akaifunga hiyo barbershop kama ilivyokuwa kwa duka la nguo.


Chege akiongea na chombo cha habari fulani alifunguka kuhusu sababu za msingi
zilizomfanya kufunga biashara zote mbili wakati wasanii wengi
wanashauriwa kuwekeza pesa zao kwenye biashara nyingine na wasitegemee
muziki tu. ”Unajua biashara ni wewe mwenyewe, biashara ni
wewe kwa maana ya kwamba unajua uchungu wa pesa uliyoweka hapo kwenye
biashara husika na unafahamu malengo yako baada ya muda flani ufike
sehemu gani. Sasa mimi ni mtu wa kuzunguka labda kwenye show au vitu
vingine vinavyohusiana na kazi yangu. Watu ninaowaacha kwenye hizi
biashara walikuwa sio sahihi kabisa. Najikuta napiga hatua mbili mbele
harafu tano nyuma. Kitu ambachi kinaniumiza mimi. Hiyo ndiyo sababu ya
kufunga duka na barbershop, sikuwa na usimamizi wa uhakika has akwa watu
niliokuwa nawaachia hizi biashara”
No comments:
Post a Comment