Breaking News
recent

Kim Kardashian ajaaliwa mtoto wa Kike, Now Kanye West anaitwa baba

Ikiwa ni wiki moja tu tangu Kanye Omario West (36) 'Kanye West' asherehekee birthday yake (june 8) mpenzi wake Kimberly Noel (32) jana (june 15) amejifungua mtoto wa kike ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya muda uliotegemewa.


Vyanzo vilivyo karibu na Kim viliuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alijifungua salama kwa njia ya kawaida (Normal child birth) na huku akiwa amewahi kwa wiki 5 kabla ya tarehe iliyokuwa inategemewa.

Vyanzo hivyo vinasema Kim alianza kujisikia vibaya siku ya ijumaa usiku (june 14) na siku iliyofuata jumamosi asubuhi alipelekwa hospitali iitwayo Cedars-sinai Medical Centre huko Beverly Hills, na kupelekwa moja kwa moja sehemu ya kujifungulia na akajifungua siku hiyo hiyo jumamosi (june 15).
                                Hapa ndiyo Cedars-sinai Medical Centre alipojifungulia Kim K
Cedars-sinai ni hospitali ambayo mastaa wengi wamejifungulia watoto wao wakiwemo Britney Spears, Jessica Simpson, Victoria Beckam na wengine wengi.

Baba mtoto Kanye West hakuwa mbali na mpenzi wake toka wanafika hospitali hapo mpaka katika chumba cha kujifungulia alikuwepo pembeni ya KK huku akishuhudia zoezi zima hatimaye mwanawe akaanza kuvuta hewa ya duniani.

Vyanzo hivyo viliendelea kusema kuwa Kanye West alilazimika kutohudhuria listening party ya Album yake mpya (Yeezus) iliyofanyika ijumaa usiku (june 14), mara tu baada ya Kim kumwanbia hajisikii vizuri ilimbidi arejee nyumbani na jumamosi asubuhi wakaongozana na mpenzi wake mpaka hospitalini.

Kim K na mwanae ambaye bado hatujajua amepewa jina gani wako na afya njema vyanzo vimethibitisha. Huyu ndio mtoto wa kwanza wa mastaa Kanye West na Kim Kardashian.
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.