Kwa muda mrefu mwanamuziki kutoka nchini Nigeria D'banj amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na mwigizaji namba moja wa kike nchini humo Genevieve Nnaji.Wote hawajawahi kukiri hadharani kuwa ni wapenzi na hivi karibuni Genevieve alionekana akiwa na pete ya uchumba kidoleni mwake jambo lililofanya vyombo vya habari nchini humo kuandika huenda akafunga ndoa hivi karibuni.
Lakini kwa upande wa KokoMaster ambae jina lake kamili ni Dapo Oyebanjo inaonyesha kama amepata kifaa kipya na kikali zaidi. Msichana huyu mrembo anaitwa Adama Indimi, binti wa tajiri nchini Nigeria aitwaye Alhajj Mohammed Indimi na mwanafunzi wa Lynn University, Florida USA.
Tetesi za watu hao kuwa wapenzi zimetokana na tweets zao na watu wengi kuanza kunong'ona kuwa huenda D'banj amempiga chini Genevieveili kuwa na Adama. August 13 2012 D'banj alitweet,"On my way to club Icon with Naeto C and the crew! Tonight, we are drinking to celebrate my babe@Presido_Adama (Adama), Happy birthday love!" August 27 2012 wakati D'banj akitumbuiza jijini London Adama alitweet picha akiwa pamoja na staa huyo backstage.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment