Breaking News
recent

Big Brother Africa: Hakeem wa Zimbabwe amwandikia 'Love Letter' Cleo wa Zambia

Ni mchezo uliojaa ucheshi, furaha, majonzi, karaha, usaliti na mapenzi kwa washiriki 24 (waliobaki) wanaoziwakilisha nchi 14 za bara la Afrika kushindania $300,000 zitakazokabidhiwa kwa mshindi mmoja tu atakayepatikana siku ya 91 ya msimu wa 8 wa reality wa show hiyo ya 'The chase'.


Ni mengi yameshajitokeza katika wiki mbili tangu shindano lianze (june 26) na washiriki wanne tayari wameshachapa lapa kutoka kwenye jumba hilo na wawili wengine watafungasha virago vyao jumapili (june 16) ikiwa ni siku ya Eviction ya wiki hii.

Tumeshaziona couple kadhaa zilizoanzisha mahusiano yao mjengoni na kila mmoja anajaribu kufanya kitu cha kumthibitishia mapenzi mwenzie. Hakeem mwakilishi wa Zimbabwe ni mmoja wao, yeye leo ameamua kumuandikia 'love letter' kipenzi chake Cleo au maarufu kama 'Ice Princess' katika ulimwengu wa muziki Lusaka Zambia.
 Kama yjuavyo katika mapenzi hata maneno matatu tu yanaweza kubadili usiku kuwa mchana (katika fikra za kimapenzi) hivyo ilikuwa ni barua yenye mistari michache tu yenye kubeba hisia nzito za Hakeem juu yake.

Kabla ya uamuzi wa kuandika barua kwa Cleo, usiku wa jana Hakeem aliapa kutojihusisha kabisa na Cleo baada ya Maria kumwambia Cleo hataki kuishi nyumba moja na Hakeem, hivyo akamueleza Maria kuwa hawezi kuendelea na msichana ambaye hampendi (akimaanisha Cleo)

Lakini asubuhi ya jumamosi (june 15) inavyoonekana moyo wa Hakeem uligundua kuwa mwili ulitikisa tu kiberiti na kuamua kubadili mawazo kisha kuamua kumwandikia barua tamu Cleo tena tamu ya herufi kubwa.
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.