Baada ya Amante kukosa ushahidi wa kutosha kwa Gary, sasa aamua
kumfuatilia katika bishara yake mpya haramu ya dawa za kulevya ili apate
sababu ya kumtupa jela Gary. Huku nyumbani kwa Alvira mahusiano yake na
Gary yanathibitika baada ya Alvira kutamka mbele ya Amante na Gary kuwa
hampendi Amante na bali anampenda Gary peke yake.
Gary anatoa maoni kwa Alvira “nikwanini tusimuondoe Amante duniani
ili aache kutuingilia penzi letu?” Alvira anashtuka na kukataa kata kata
na kumwambia Gary asijaribu kuingilia na kumdhuru Amante kwani huo ni
ugomvi wao, na pia Amante bado ni mumewe wa ndoa. Alvira anaanza
kuutambua moyo wa Gary kwa matendo anayoanza kumuonyesha.
Gonga continue reading kuendelea..
Gary anaanza kama kumlazimisha Alvira wanyonyane ndimi, pia ahamie kwa Alvira, lakini Alvira kwasababu malengo yake sio kuolewa na Gary ni kutafuta vidhibiti vya maovu ya Gary, hivyo anamwambia Gary asiwe na haraka ya mambo, muda utafika tu.
Gary anaanza kama kumlazimisha Alvira wanyonyane ndimi, pia ahamie kwa Alvira, lakini Alvira kwasababu malengo yake sio kuolewa na Gary ni kutafuta vidhibiti vya maovu ya Gary, hivyo anamwambia Gary asiwe na haraka ya mambo, muda utafika tu.
Huko kijijini Suzan anapata vipimo kuwa ni mjamzito, ujauzito
unaosemekana kuwa ni wamumewe Gary. MARA adhamilia kabisaa kurudi
nyumbani kwao, lakini Alvira anamsihi Suzan amzuie kwani huko mambo
bado sii mazuri. Huku mjini Clara nae amerejea tena huku akiendeleza
kumfanyia bibi yake ugaidi.
Mama yake Gary anapata nafuu ya kuweza kutembea japo kwa shida, hadi
alikochimbia zile fedha za Gary. Akiwa bado anachimbua, mfanyakazi wake
anaanza kumtafuta huku akisaidiana na CG,wanamkuta japo alikuwa bado
hajazitoa.
Amante anajipanga yeye na wenzake ili kumfuatilia Gary katika
biashara zake za dawa za kulevya, anafanikiwa kuchukua video kwa njia ya
simu, lakini wenzake Gary wanashtukia kuwa kunamtu anawafuatilia, hivyo
wanamwambia Gary. Amante akiwa bado ananyata kuondoka mara Gary
anatokeza kwa nyuma yake na bastora na kusema “Amante leo sitokuacha,
huwezi kuondoka”, Gary anampiga risasi na Amante kuanguka chini.
Nyumbani kwa Gary yeye na Clara wanafanikiwa kuzifukua zile pesa
zilizokuwa zimefukiwa na mama yake. Amante afanikiwa kufikishwa
hospitali, huku Suzan na MARA wafanikiwa kurudi na kufika hospitali
kumuona Amante.
Gary anafika hospitali na kumkuta Suzan na MARA, anatoa bastora na
kumnyoshea Suzan lakini Alvira na MARA wanamzingira Suzan kwa pamoja,
mara Gary bado akiwa na hasira anawauliza “mnafikiri mtakimbia kwenda
wapi?” anawaonyooshea bastora wote watatu. Huku Madaktari wanajaribu
kumpiga shoti Amante ili azinduke lakini juhudi kama zinagonga mwamba
hivi!
Mwandishi: Mohamed Jaku (www.mohamedjaku.blogspot.com)
To be continue......
No comments:
Post a Comment