Orodha ambayo inaonyesha wasanii wa kike wa filamu 15 ambao wana vipato
vya juu kabisa imetoka ikiwa pia inaonyesha kiasi cha pesa ambacho
wanadada hawa hujitengenezea, huku nafasi ya kwanza ikiwa inashikiliwa
na bibie Genevieve Nnaji.
Genevieve anafuatiwa kwa karibu sana na Ini Edo, Patience Ozokwo,
Omotola Jalade, Kate Heshaw, Stella Damascus, Joke Silver, Ngozi Ezeonu
na Rita Dominic, ni kati ya wale mastaa ambao kumuweka katika picha
yako, utatakiwa kumlipa zaidi ya Naira Milioni 1, zaidi ya shilingi
milioni 10 za Tanzania.
Wengine katika orodha hiyo wamo Chioma Chukwuka, Oge Okoye, Funke
Akindele, Mercy Johnson, Fathia Balogun na Uche Jumbo ambapo ni katika
kundi la mastaa mbao dau lao halishuki chini ya Naira laki 4 na nusu,
zaidi ya shilingi milioni 4 na laki 6 za Tanzania.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment