Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba
muigizaji maarufu wa sanaa za vichekesho Hussein Mkiety maarufu kama
SharoMillionea amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Akizungumza na simu na Millard Ayo wa Clouds FM RPC wa mkoa wa Tanga alisema: "“leo majira ya saa mbili usiku
kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la
Hussein Ramadhani Mkiety au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR
Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo
gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo
chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya
ya Muheza.”
Kwa taarifa zaidi endelea kutembea mtandao huu kujua taratibu za mazishi za msiba huu mkubwa kwenye tasnia ya burudani nchini Tanzania
Bongo Forest
Ajali
News
Sharo millionea
Breaking News: Muigizaji Sharo Milionea afariki kwa ajali ya gari

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment