Baada ya kukaa kwa muda mefu pande za UK
na hivi majuzi kuingia kwenye ardhi ya Jakaya, Najma Dattan
commonly known as Naj aamua
kuingia kwenye tasnia ya filamu za kibongo maafufu kama
Bongo Movies.
Msanii huyu ambaye ameshafanya ngoma kali katika upande wa Bongo flavour
kama “Dont Let Me Go” akiwa na X-boyfriend wake Herry
Sameer alias Mr.Blue
na sasa anatamba na ngoma iitwayo “Lets Dance” aliyompa
collabo mkali AY, rasmi amuamua
kuingia kwenye kiwanda cha movie za Bongo.
Latest Infoz toka kwa Naj ni kuwa ameshafanya mazungumzo na kampuni
inayokgwenda kwa jina la Rj Company iliyo chini na Vicent
Kigosi alias Ray kuanza kufanya movie hiyo. Movie hiyo inaitwa “Superstar”
na siku ya kesho ndio wataingia kampini kwa ajili ya kuanza kushoot movie hiyo.
Hivyo mashabiki wa Naj
mkae mkao wa kula kuona kama msanii huyu ataweza kukinukisha vizuri kwenye
upande wa filamu kama alivyoweza kufanya poa
kwenye music.
No comments:
Post a Comment