Msemaji wa kundi la Weusi Nikki
wa Pili ametoa kauli ya kwanza toka kukamatwa kwa Lord Eyez wa kundi
hilo kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz.
Namkariri Nikki wa Pili akisema
“kwanza hiyo ni habari ya ghafla alafu ni ya kusikitisha na kushtua, ni
habari ambayo imetupa shida na mpaka sasa inatupa shida sana kwa sababu
watu wengi wanatupigia simu kutuuliza inakuaje”
“Ukiangalia kwenye mitandao ya
facebook na twitter kote imesambaa, unajua ukijua ukweli ni kitu cha
msingi sana kwa sababu sisi pia tulikua hatufahamu kilichotokea, kwa
hiyo cha kwanza tulichokifanya ni
kutaka
kujua kilichotokea, mfano mimi niliona kwenye mitandao kwamba Lord Eyes
amekamatwa kwenye eneo la tukio yupo kwenye gari lakini kufatilia
nikaja kugundua haikua eneo la tukio na sio gari hilo, uhalifu
ulifanyika alhamis na alikamatwa jumamosi” – Nikki wa Pili
“Kitu cha busara tulichoamua
kufanya tumeamua kufatilia kisheria ili tujue uhalisia ni upi ili tuweze
kutoa tamko kwa sababu sisi wenyewe Lord Eyez hatujamuona wala
hatujaongea nae, na kingine ambacho kinasikitisha ni kwamba Lord Eyez
ndio ametuhumiwa kama mtu binafsi lakini ukiangalia kwenye mitandao watu
wanawashambulia weusi kitu ambacho sio sahihi kabisa, mimi Joh Makini,
Bonta, G Nako tumepokea hiyo habari kama mtu mwingine yeyote” – Nikki wa
Pili.
No comments:
Post a Comment