Pancho kufanya kazi na Camp Mulla na Octopizzo
Ni moja kati ya ma producer wakali hapa Tzee wanaotamba kwa kugonga
ngoma kali ambazo zinafanya mpaka dzain raia wa hapa bongo land wanasema
duuuh!!!!!! kweli huyu producer ni noma najua wajua namzungumzia nani
huyu si mwingine anajulikana kwa jina Pancho Latino kutoka Label ya B hits kwa mtu mzima Hammer B.Habari
ambayo tumeipata hivi sasa kwamba producer huyu anatarajia kufanya kazi
na wasanii ambao kiukweli kwa sasa dzain ndiyo wana hits na ngoma zao
kali kadhaa kule pande za 254 hawa si wengine nawazungumzia Camp mulla na Octopizzo.Producer
huyu anatiririka kama ifuatavyo kuhusiana na habari ambayo tumeipata
kwamba anatarajia kufanya kazi na Camp mulla na octopizzo huyu hapa"
Yap ni kweli natarajia kufanya nao kazi za muziki kwani kwa sasa ndiyo
tupo katika michakato ya mazungumzo kwa hiyo napenda kuwambia wale
mashabiki wangu wakae tayari kwa kusikia kile ambacho nitakacho wafanyia
Camp mulla na Octopizzo"Hayo ndiyo maneno ya mtu mzima Pancho
Latino akifunguka kuhusiana na Camp mulla na Octopizzo kama unavyoona
amesema kwamba ndiyo dzain wapo katika mazungumzo ya kuweza kufanya nao
kazi kwa hiyo basi tunamtakia mafanikio mema na kazi nzuri atakayo
ifanya wasanii hao.
No comments:
Post a Comment