Mara zote tangu nianze kulisikiliza tangazo la "TUKO WANGAPI" na kuliona
kwenye luninga, nimekua nikisisimuka na hasa kuchukua dakika kadhaa
kujiuliza hivi kweli tuko wangapi?.
Jana katika kumalizia weekend yangu, nilikuwa na washkaji maeneo
tukipiga soga, na bila kujua tukafikia maongezi yaliyokuwa yanawahusu
wadada zetu wanaokaa mabarabarani kwa minajili ya kujiuza, stori
ziliendelea na mwisho wake kila mmoja alibaki kimya huku akionyesha
kuwaza maisha haya tuliyonayo kwa sasa.
tukiachana na hayo ambayo tunauwezo wa kuyaepuka kwa kuwa muaminifu, hii habari ndio imenifanya kuandika hiki niachokiandika
zimepita takribani wiki nne tangu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi alipojitangaza
kuwa ni HIV positive na aliapa kuwa lazima ausambaze kwa watu kwasababu
aliupata ama aliambukizwa wakati alipofanya tendo la ndoa kwa mara ya
kwanza
"nimeshalala na wanaume 322 katika campus yangu na wawili kutoka
nje.Nilitaka kuwaambukiza watu 2,500 lakini dhamira yangu inanisuta na
inaniumiza moyoni".alisema mschana huyo
cha kusikitisha zaidi report hii imekuja miezi miwili tu baada ya
msichana mwingine mwanafunzi wa chuo kikuu cha Moi kutoa list ya ya
wanaume 90 na kuzibandika kweye notice board akidai amewaambukiza wote
virusi na katika list hiyo kulikua na majina mawili ya wanasiasa maarufu
nchini Kenya.
msicha huyo amekua na uchungu hata kufikia uamuzi huo wa kuwaambukiza
wanaume 322 kwasababu aliambukizwa ugonjwa huo katika siku yake ya
kwanza ya kungonoka.
swali nililobaki nalo hapa ni TUNAELEKEA WAPI? VIPI HALI YA VYUO VYETU HAPA BONGO?
No comments:
Post a Comment