Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu Irene Uwoya amchafue mpenzi wake wa zamani, H-baba kua hana lolote kitandani msanii huyo wa bongoflava ameamua kusema sababu halisi ya kuvunjika kwa uhusiano wao.
Akiongea na kipindi cha XXL cha clouds fm jana kwa sauti iliyoonesha ghadhabu ndani yake, H-baba alisimulia kua alimpa ujauzito Irene na kumsisitiza kuwa asiitoe kwani angependa kuwa na mtoto.Alisema siku moja Irene alimwamboa mpenzi wake huyo wa zamani kuwa anajisikia vibaya hivyo akampeleka dispensary ili akachukuliwe vipimo aanze dozi.
H-baba ambaye jina lake la kwanza ni Hamis alidai baada ya kufika hospitalini na Irene kumuona daktari alishangaa kuona mpenzi wake amekaa kwa muda mrefu kwenye chumba cha daktari, alisema alipotoka Irene alionekana amelegea isivyo kawaida na ndipo Irene alipomwambia ukweli kuwa amechomoa mimba.
Kitendo hicho kilimuumiza sana Hamis ambaye alidai kuwa kila mmoja alirudi nyumbani na njia yake na huo ndio ukawa mwishi wa penzi lao.Alisema kilichomkera zaidi ni kuwa, Irene aliandika jina lake (Hamis) kwenye kadi ya hospitali, "Je kama angekufa ingekuaje?" alisema H-baba.
No comments:
Post a Comment