
Maelezo ya Dogo Janja yanasema kwamba juzi (September 2) walivyokua Club Maisha aliperform
akiwa na furaha kutokana na mashabiki zake waliojitokeza na alipomaliza
kuperform alishuka kwenye stage akiwa na furaha baada ya kufanya vizuri
lakini hiyo furaha ilikatishwa baada ya kwenda juu sehemu ya V.I.P
Janja anasema alipopanda V.I.P
kumsalimia Producer Maneck alimjibu kwa dharau na kumwambia haongei na
Masnich hivyo Dogo Janja akaondoka lakini muda mfupi baadae alirudi na
kukuta Tunda Man yuko karibu na alipokaa Maneck, Janja pamoja na Tunda
walimsogelea producer huyo ambae alianza kumtukana matusi mazito Dogo Janja.
Baada ya hapo ilibidi Dogo
Janja kushuka chini na kwenda kumchukua Ustaz Juma ambae ndio boss wa
kundi alilopo sasa Dogo Janja la Watanashati, walipofika alipo Maneck..
alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja aliyorekodi na producer Marco
Chali kwa kusema wimbo huo ambao mwanzo ulikua urekodiwe kwa Maneck ni
wa kawaida sana.
Kwenye
line nyingine namkariri Dogo Janja akisema “nikawa nimepanic sana sasa
leo nakuja kupokea simu eti Tunda man nae anasema nifute chorus ya
‘Anajua’ kwenye wimbo wangu, Bro ule wimbo nimeurekodi nikiwa Tip Top na
nimeifanyia show nyingi sana Tanzania ambazo zimewaingizia hela nyingi
sana, hawana ubinadamu yani wanaponiambia mimi nifute chorus, Tunda
kawafanyia watoto wangapi chorus? Shetta, Pasha lakini mbona hamwaambii
Pasha afute au labda sababu mi mdogo, hili swala nawaachia watanzania
kwa sababu ile ni haki yangu, nilimshirikisha Tunda.. ule wimbo sio wa
Tunda siwezi kufuta chorus”
Baada
ya hayo maelezo ya Dogo Janja, Producer Maneck amezungumza exclusive na
millardayo.com na namkariri akisema “Dogo Janja alikuja akanisalimia
nikamwambia ebwana eeeh kaa mbali na mimi sihitaji kuongea na wewe kwa
sababu unatabia za kisnich sana, kuna vitu flani alivifanya siku kadhaa
zimepita na sikupendezwa navyo.. tuliandaa show ya Tunda Man pale Maisha
Club tukamwambia na akakubali kufanya na tukatangaza kwamba atakuepo
sasa mwisho wa siku akabroadcast msg kwenye BBM alafu sisi hakututumia
ile msg ila akabroadcast kwa watu kwamba hao ni matapeli, hapohapo
nachat nae namuuliza mbona umezingua anasema mi naona aibu sijui hata
sura yangu sijui nitaiweka wapi kwa bwana Captain, huku anasema hivi
huku anafanya hivi”
Tunda Man nae ametoa sababu za
kumwambia Dogo Janja afute sauti yake kwenye kolabo waliyofanya ya
‘Anajua’ na nina mkariri akisema ” sikuzungumza kwa ubaya, nimezungumza
kwa nia nzuri tu.. kwenye chorus inasema niko na Captain Tunda man alafu
mimi siko pale mashabiki wanakua kama hawakuelewi vizuri, kuna mistari
mingine inasema narun city nikiwa na JCB, narun Dar City nikiwa na T.I.P
sasa ujue kwenye show kuimba vitu kama hivyo wakati hayupo na Tip Top
vinakua havileti maana, ni kama maoni tu nimemuomba aimbie beat kwa
sababu anaweza kurekebisha ile mistari, mfano kusema narun city nikiwa
na Watanashati, kwenye show ndio abadilishe lakini kwenye audio ni sawa
ikibaki na vionjo vya mwanzo”
No comments:
Post a Comment