Gazeti
la the Sun limeandika line chache na nzito kuhusu maamuzi mapya ya
Mchezaji ASAMOAH GYAN ambae amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja
kutoka Sunderland kwenda kucheza soka lake United Arab Emirates akiwa
tayari amekipiga kwa mkopo na club hiyo ya Al-Ain kuanzia msimu
uliopita.
Mshkaji huyu Mghana alijiunga na Black Cats kutokea Ufaransa kwa ada ya pound milioni 13 mwaka
2010
na alifunga magoli 11 kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya English
football, pamoja na kufanya uamuzi wa kwenda kucheza U.A.E amesema
anajua watu watamkosoa lakini anaifanya kazi yake, alilijadili hilo na
familia yake na ikakubali, ni maisha yake.. anachotaka ni kwenda kucheza
soka la kiwango.
No comments:
Post a Comment