Rapper Bill Nas amesema kuwa kufanya video ya wimbo wake Mazoea Bongo
badala ya Afrika Kusini, hakujaokoa gharama yoyote. Amedai kuwa licha ya
video hiyo kufanyika nyumbani, imetumia gharama kubwa zaidi.
Amesema kile ambacho amekiokoa ni muda tu kwakuwa kama angesafiri kuna vitu vya nyumbani ambavyo angeviacha ‘pending.’
“Lakini kwenye suala la pesa video ya Mazoea imezidi gharama hadi
video ya Chafu Pozi, imezidi sana. Labda kama ningeenda kuifanya kule
gharama labda zingezidi sababu ilikuwa ni collaboration labda gharama za
kumsafirisha Mwana FA makazi yake kule na vitu vingine, halafu
tungesafiri na timu kubwa pia,” Bill Nas amemuambia mtangazaji wa Pride
FM ya Mtwara, Eddy Msafi.
Video ya Mazoea imeongozwa na Msafiri.
Bongo Forest
Billnas
Mwana FA
Video
Video ya Mazoea imenigharimu zaidi kuliko ya Chafu Pozi – Bill Nas

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment