Breaking News
recent

Umuhimu wa hii tuzo ya Next Rated umesababisha kugombana kwa Olamide na Don Jazzy.

Korede Bello mwimbaji wa Marvins records ameongelea msanii mwenzake Reekado Banks kushinda tuzo ya Next Rated.

Tuzo ya Next Rated ya Headies ni tuzo inayopewa kwa msanii anayetegemewa kuwa staa na kuwa na mafanikio makubwa zaidi miaka ijayo,hii ni tuzo muhimu sababu wote walioshinda wamekuwa na mafanikio.
Korede Bello Anasema “Reekado Banks amefanya kazi sana mwaka 2015 na anastahili kuishinda tuzo hio,msanii mwingine ni Kiss naye kafanya vizuri na Lil Kesh, ila isiwe issue kubwa kama unakosa tuzo hii sababu ni kura za mashabiki ndio zinakupa ushindi” .
Kuhusu sababu ya yeye kuto andika chochote mtandaoni kuhusu issue hii Korede Bello anasema “Nasomea Mass Communication kwenye chuo cha Nigerian Institute of Journalism, siwezi kuongea au kusema kitu kuhusu issue ambayo ndio kila mtu anaongelea kwa wakati huo”.
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.