Kupitia page yake ya Instagram @Idris Sutlan kafunguka na kusema haya kuhusu Wema…
>>> “ Mimi
na wewe sio kama watu wengine. Nalala, nakula na naamka nikiwa
nakufikiria wewe. Unafikiri una bahati ya kuwa na mimi ila hapana hapana
mimi ndio mwenye bahati ya kuwa na wewe. Mara ya kwanza ilikuwa ajabu
kwangu kuangalia ndani ya kabati langu la nguo na kuona nguo zako na
viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia “Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike“
au ukiingia jikoni kwangu na kuitawala nyumba yangu na vyakula vizuri.
Jinsi unavyowatazama wanawake wengine wakinisogelea, jinsi vile
unavyojua ni wakati gani nahitaji kupewa a kiss au kumbatio zito. Jinsi
unavyonilazimisha kuangalia channel ya Disney, jinsi unavyoniamsha
mapema siku hizi kunitengenezea chai. Naweza nikakuletea ua zuri la
waridi lakini halitaweza kufikia uzuri wako. Ukiwa na wivu unasonya
sonya, nikiwa na wivu natabasamu. Naweza kufanya lolote hata kuhamisha
milimia kwa ajli yako. Nitakulinda, nitakupenda, nitakudekeza,
nitakupikia, nitagombana na wewe, tutaangalia movies pamoja, nitakaa na
wewe kuangalia nyota. Wewe ni zaidi ya kile nilichokiomba, wewe ni kila
kitu changu “My Wife”. <<< @idrissultan

No comments:
Post a Comment