Breaking News
recent

Weusi Waeleza Sababu za Kwanini Mwaka Huu Hawajoa kazi ya Kundi

Kundi la Weusi linaloundwa na G Nako, Joh Makini, Nikki wa Pili, Lord Eyes na Bonta limeeleza sababu za kwanini mwaka huu hawajatoa kazi ya pamoja as kundi. Mbali na single za mmoja mmoja ambazo hata hivo kila mmoja zimemsaidia kumuweka pazuri zaidi.


Baadhi ya nyimbo walizotoa Weusi kama mmoja mmoja mwaka huu ni kama "Joh Makini - Nusu Nusu na Don't Bother", Nikki wa Pili ametoa "Safari" na "Baba Swalehe", G Nako ametoa "Laini" na anatarajia kutia wimbo mpya hivi karibuni uitwao "Original" na Bonta anategemea kutoa kazi mpya.

Msemaji wa kundi hilo Nikki wa Pili amekiambia chombo kimoja cha habari sababu za kutotoa kazi ya kundi mwaka huu:-
"Mwaka huu Weusi hatujafanya kazi ya kundi ukiacha Gere ya mwaka jana. Sisi msingi wa kundi letu ni kutengeneza msanii mmoja mmoja na sio kundi, mkitengeneza sana brand ya kundi na mkasahau individuals kundi likija kuanguka basi wote mnaanguka, halafu sisi hatutaki hiyo ije itokee. Nikki wa Pili anatakiwa uwepo wake usitegemee uwepo wa Weusi au Joh Makini uwepo wake usitegemee Weusi na G nako vile vile. Kwahiyo sisi individuals kwanza then kundi".

Nikki aliendelea
"Kwa mwaka huu plan ya kundi ilikua ndogo sana kulingana kulikua na project za mtu mmoja mmoja na mazingira ya kampeni pia yalichangia. Mwaka huu Weusi waliplan kazi za mtu mmoja mmoja".
Alimalizia Nikki..
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.