Muimbaji wa DanceHall kutoka Nigeria, Burna Boy ameponda mfumo wa mziki wa Nigeria kwa kudai kuwa umejaa siasa na ndio maana hapati tuzo nyingi anazostahili.
Akizungumza na jarida la Fader, Burna amesema kutokana na hayo anajiona kama yeye si sehemu ya mziki wa Nigeria kwasababu kuna baadhi ya watu walioutawala mziki huo wasiompenda.
"Kusema kweli ni siasa tupu, sijaona kama ni sehemu ya kiwanda cha mziki. Angalia tuzo, sipati tuzo kwasababu walioutawala huu mziki hawanipendi, mimi sio kama wengine, siwezi kufanya kama wafanyavyo wengine, hawapendi hicho".
Muimbaji huyo wa "Check and Balance" ameongeza kuwa licha ya kuwa hana wafuasi wengi Instagram na Twitterlakini anaamini anafanya vitu vizuri na vikubwa kuwazidi wasanii wengine wenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii".

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment