Rnb staa Chris Brown ametoa maelezo ya kwanini halipishi wasanii
ilikufanya nae collabo ikiwa ni tofauti na wasanii wengine nchini
Marekani kama 2 Chainz ambaye huchaji mpaka dola laki moja kwa collabo
moja.
Chris Brown anasema “sichaji pesa
wasanii wenzangu sababu naandikia wasanii wengi na collabo nyingi nazo
fanya na wasanii hao ni wasanii waliowahi kunasaidia kwenye nyimbo zangu
so nikama narudisha fadhila tu, pesa nayopata kwenye collabo inatokana
na mauzo ya wimbo kama single na mitandaoni, nakuwa nimeandika mashairi
mwenyewe so napata asilimia yangu hapo “.
Sababu nyingine ya Chris Brown kutopenda kulipwa kwa collabo ni kuwa
anapenda kujenga na kudumisha uhusiano mzuri na wasanii wenzake.
Chris Brown pia alisema “ kwa wasanii
wanaochipukia huwa anatanguliza pesa yake anayotaka ya kufanya nao
collabo sababu wimbo atakao fanya na msanii huyo utamtambulisha vizuri
kwenye muziki na ni muhimu msanii kuthamini brand yako “.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment