Mengi yamezungumzwa juu ya kinachodaiwa kutengana kwa kundi maarufu
Africa kutoka Nigeria "PSquare" huku wengine wakidai kuwa ni
kutokuelewana kwa Petter na kaka yao mkubwa ambae ndio manager wao "Jude
Okoye" huku wengine wakitupa lawama kwa mke wa Petter "Lola" kuwa ndio
chanzo maana hata mama yao alipokuwa hai hakupenda Petter amuoe mwanamke
huyo ambae licha ya kuwa amemuoa baada ya mama yake kufariki, Kaka yake
"Jude" hakuhudhuria harusi yao pamoja na kuwa alikuwepo nchini Nigeria
Leo hii kupitia mtandao wa onlinenigeria umethibitisha sababu za ugomvi
mkubwa uliotokea kati ya kaka hao ndugu ambao ni mapacha.
Inasemeka kuwa ugomvi huo ulianzishwa na wasaidizi
wao(Personal Asisstants). Msaidizi wa Jude alimpa pesa msaidizi wa
Petter akamsajilie gari lake, lakini msaidizi wa Petter hakufanya hivyo
badala yake akatumia pesa hizo kwa matumizi mengine.(na ndio kijana
alieripotiwa kula pesa zilizokuwa zikanunue gari la marehem mama yao
alipokuwa hai)
habari ikaendelea kuwa msaidizi wa Jude akakasirika sana baada ya kuona
pesa zake hakuna na gari lake halijasajiliwa ndio akaamua kumfata
msaidizi wa Petter aliekuwa nyumbani kwa kina Psquare (Squareville) ,
alipofika wakaanza malumbano na kufikia ugomvi mkubwa baina yao, mpaka
kufikia kutoana damu, ugomvi ukawa mkubwa kiasi kwamba Petter akaingilia
ugomvi na kutaka kumpiga msaidizi wa Jude ndipo Paul nae akaingilia na
kumshika mkono kaka yake kwa ajili ya kumzuia.
katika stage hiyo ya ugomvi Petter alizungusha mkono wake na kumpa kitu,
inauma Paul mpaka akaanguka chini .Inasemekana Paul hakumrudishia ngumi
ila kaka yao mkubwa "Tony" aliingilia na kuanza kumpiga Petter.
Kwa kile kinachodaiwa na chanzo hicho cha habari ni kuwa Petter anataka
kuwa in-charge wa pesa zao, kaka yao mkubwa na manager wao Jude siku
zote amekuwa akisimamaia swala hilo huku Paul akitaka iendelee kuwa
hivyo hivyo.
ishu ilikuwa imefikia pabaya mpaka kuamua kumleta wakili kwa ajili ya
kugawana mali zao, lakini mwisho wa siku hakuna aliesema hiki na cha
yule na hiki ni changu na wakili kushindwa kuendelea.
Tweet ya kaka yao "Jude" na Manager iliwashtua sana mashabiki wa PSquare duniani baada ya kuandika "after ten years am done"
lakini Paul amevunja ukimya kwa kuandika katika ukurasa wake wa facebook,
"After the storm comes the calm, hoping for better days ahead as one familly.Gods intervention"
No comments:
Post a Comment