Siku moja baada ya kutimuliwa kutoka kwenye kibarua cha kuifundisha
klabu ya Manchester United imefahamika kwamba kocha David Moyes atalipwa
fidia kutokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wa miaka sita walioingia
mwaka jana mwezi wa tano.
David Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na
Manchester United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake
na klabu hiyo.
Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele kinachoeleza
ikiwa Manchester United ingefeli kufuzu kucheza Champions League msimu
huu basi ikatokea United wakaamua kusitisha mkataba wake basi fidia
isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment