Msanii wa Hiphop anaeiwakilisha Ilala, Chidi Benz anadaiwa kushikiliwa
na polisi mwishoni mwa wiki baada ya kumpiga na kumjeruhi vibaya
mwanadada anaejulikana kama Mwanaisha ambae anadaiwa kuwa ni mpenzi
wake wa zamani.
Kwa mujibu wa Chidi Benz amesema yeye alikuwa akipita nje ya bar iliyo
karibu na kwake ilala Flat alipokuwa akirudi nyumbani kwake akiambatana
na mpenzi wake wa sasa ndipo aliposkia sauti ikimuita na kumuuliza zaidi
ya mara tatu
" chidi naona uko na mama watoto" kusogea karibu akakuta ni Mwanaisha na
wenzake, ndio akamwambia mbona unanichora au kwasababu nipo na dem
mkali kuliko wewe unaona wivu, kilichofata ni chupa ambayo Mwanaisha
aliirusha ikampata kichwani na kumpasua damu zikatoka ndipo yeye
alimshika nywele Mwanaisha na baada ya hapo kilichofata hakumbuki maana
alikuwa amelewa.
Chidi Benz anashikiliwa na polisi na leo hii kesi imeenda mahakamani
ambapo hakimu ameamuru kuendelea kushikiliwa kwa Chidi baada ya hali ya
mwanaisha kuwa mbaya kiasi cha kushindwa kuongea.
Mwanaisha ameshonwa nyuzi 18 mdomoni, uso umeumuka na kichwa kimemvimba sana.
Mwanaisha mwenyewe huyu hapa akiwa hospitali
No comments:
Post a Comment