Msanii wa Kufoka foka hapa Bongo Richard Alibalio aka M Rap wiki
kadhaa zlizopita ali-make headline kwenye mdeia za hapa Tanzania
kutokana kuibuka ugomvi kati yake na aliyekuwa msimamizi wa kazi zake
na ndiye producer wa BHits Pacho Latino.
M Rap kwa sasa ana ngoma moja mpya inafahamika kwa jina la ‘Usiende
Mbali’ aliyomshirikisha Jux aliufanya kwenye studio ya AM Records
producer ni Maneck baada ya kutoka BHits right now MRap ametoa kauli
yake ya mwisho kwa mabosi wake wa mwanzo.
“Nashukuru Mungu nimeishi vizuri na watu nilikuwa nafanya nao kazi
kama Vanesa, Jux na wote tuliokuwanao lebo moja, mimi moyo wangu upo
safi kabisa na nashukuru coz nimejifunza mambo mengi na kila kitu huwa
kinatokea kwa sababu.
Alisema “Kwa sasa nipo chini ya Maneck ambapo nilipokuwepo mwanzo
kabla B hit hawajaniona na wala sikuondoka kwa ugomvi so nimerudi
wamenipokea kwa mikono salama na kwa sasa siko tayari kwenda mahali
pengine bila kuwa na uhakika wa kufanya kazi na watu serious.”
Alimalizia kwa kusema “Kiukweli ni ngumu sana kufanya kazi na mtu
ambaye hautakuwa na uhuru na anayejiona muhimu kuliko wewe wakati
tunaishi kwa kutegemeana, asante kwa mashabiki wangu ambao bado wapo na
mimi bega kwa bega so wategemee mambo mazuri kutoka kwangu.”

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment