Breaking News
recent

Official: Juan Mata afaulu vipimo na kujiunga rasmi na Manchester United

Manchester United imekamilisha rasmi usajili wa kiungo Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya usajili ya £37.1 million, ambayo ni rekodi mpya katika usajili wa United, klabu hiyo imethibitisha.

Mata, 25, ameshaichezea mara 32 timu ya taifa ya Spain na amecheza mechi  135 Chelsea, akifunga mabao 32 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Valencia mwaka 2011.
Juan Mata alinukuliwa na mtandao wa Man U akisema: “Nina furaha sana kujiunga na United. Nilikuwa na muda mzuri sana Chelsea lakini muda umefikia kwa changamoto mpya. United ni sehemu sahihi kwangu na nina shauku kubwa ya mmoja ya waliopo katika historia mpya ya klabu hii.
“Chelsea ni timu kubwa na nina marafiki wengi pale lakini huwezi kukataa nafasi ya kujiunga na Manchester United.” – Mata
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.