Mara baada ya tetesi kusambaa sana mitaani na kwenye mitandao juu ya
Diamond kununua ndinga mpya mara baada ya kuonekana aki-post picha akiwa
na gari hilo bila neno lolote yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 245 za Kitanzania hatimaye Chief Kiumbe amefunguka juu ya ndinga
hilo.
Leo asubuhi kupitia interview na kituo flani mfanya biashara ‘Chief
Kiumbe’ alifunguka na kusema kwamba gari analomiliki msanii wa bongo
fleva ‘Diamond’ ni la kwake.
Huu ndio ujumbe wake Chief Kiumbe.
“Unajua mimi huwa sio mtu wa kuzungumza sana ila ukweli ni kwamba
wasanii wengi wa hapa bongo wanatembelea magari yangu, na wala hawatoi
hela yoyote,kwa mfano Diamond anamiliki gari yangu mpya ambalo nilinunua
zaidi ya shilingi milioni 245 kipindi niko nje kiziara, nafanya hivi
kwasababu ya upendo na pia wapo wasanii wengi tu, kuna wengine
wanajitamba kwamba wamenunua ila sio kweli mimi ndio ninawapa bureee
watembele hizo habari za kwamba wananunua hakuna kitu kama hicho,mimi
napenda watu wafuate nyayo za Diamond naamini watafanikisha ndoto zao” –
Kiumbe.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment