Forbes.com wametoa list wasanii wa Hiphop ambao wameingiza pesa
nyingi sana kwa muda wa miezi 12 iliyopita. List imeanza na msanii
tajiri kuliko wote kwenye muziki wa Hiphop na kuna mwanamke mmoja tu
ambaye yupo kwenye hii list.
1. P. Diddy
Forbes wameandika kwamba Diddy ameingiza zaidi ya dola millioni 50
kwa muda wa miezi 12 iliyopita. Vyanzo vyake vikubwa ni Ciroc
Vodka,Sean John,Bad Boys, Blue Flame agency pamoja na mkataba wake mpya
na Warner Cable kwa ajili ya Revolt TV
2. Jay Z
Jay Z ameingiza dola millioni 43, vyanzo vyake vikubwa ni Armand de
Brignac champagne, D’Ussé cognac, Roc Nation label/management firm. Pia
album yake ya Magna Carta Holy Grail ambayo Samsung waliweka investment
ya dola millioni 5. Pia Jay anabiashara nyingine kama uwakala wa
wanamichezo mashuri kama Kelvin Durant na pia aliuza share zake za
Brooklyn Nets.
3. Dr Dre
Ameingiza dola millioni 40.Kama kawaida ya Dr Dre, pesa nyingi
anavuta kutokana na headphones na earphones za Beats by dre. Pia
anafanya upanuzi wa kampuni zake nyingine
4.Nicki Minaj
Ame-gross dola millioni 29, mwanamke pekee kwenye list amepata pesa
hizi kwenye show nyingi anazofanya, mkataba wake wa Ameican
Idol,mikataba yake na vinywaji kama Pepsi.
5.Birdman
Pesa alizongiza ni dola millioni 21, record label yake inawasanii
wakubwa kama Lil Wayne,Drake na wengine. Pia vyanzo vingine ni kama nguo
za YMCMB,Vodka na publishing.
6.Kanye West
Mkali wa Yeezus ameinginza dola millioni 20, album yake mpya ni moja
ya vyanzo vikubwa sana kwake. Pia Kanye anamikataba,show nyingini na
clothing line ya Donda West.
7.Lil Wayne,
Lil Wayne ameingiza dola millioni 16, show,Young Money na nguo za Trukfit ni vyanzo vikubwa kwake
8.Wiz Khalifa
Dola millioni 14 zimeingia kwenye account yake, show zaidi ya 75
baada ya nyimbo zake kufanya vizuri ndiyo vyanzo vikubwa vya pesa zake.
9.Ludacris
Mkali wa fiesta ameingiza dola millioni 12, vyanzo ni headphones za Soul by Ludacris,show zake na role yake kwenye movie ya FF6.
10.Pitbull
Fungu lake ni dola millioni 11 ambapo zinatokana na album yake ya Global Warming, tours na endorsements na Kodak pamoja na Dr. Pepper.
No comments:
Post a Comment