Breaking News
recent

Ommy Dimpoz asaini mkataba tour ya Canada na USA

Omary Faraji au al-maarufu kama Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo  hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu.
"yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz
alipomuuliza na mwandishi wa habari kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 
"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa? .
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.