Ni muda umepita hatujasikia story kuhusu washiriki wa Tanzania katika Big Brother toka Feza aponee chupu chupu kuiaga $300,000. Lakini kipenzi cha kinadada kijana mtanashati 'handsome' Nando ameibuka na lake baada ya kuonesha hitaji la kuondoka South Africa akiwa na kumbu kumbu ya mchoro katika mwili wake(tattoo).
Wakati wenzake mjengoni wanakimbizana na mapenzi yeye mapenzi yake hivi sasa ni juu ya mwili wake kupata mchoro 'tattoo'. Akiwa kwenye Diary session Nando alimuomba Biggie amletee mtu wa kumchora tattoo mjengoni, baada ya ukimya bila kumuona mchoraji huyo Nando akiwa kwenye diary session nyingine alimkumbusha biggie juu ya ombi lake la kuletewa mchora tattoo.
Well, inavyoonekana ugonjwa wa tattoo baada ya kukosa tiba ya haraka kwa mgonjwa wa kwanza (Nando) hatimaye virusi vikaanza kwa mshiriki mwingine wa Botswana Motamma ambaye alimuunga mkono Nando baada ya kumwomba na yeye biggie amfanyie favor ya kumletea wa kumchora tattoo mjengoni.
Siku Nando akirejea Tz iwe na kitita cha $300,000 au laa ukiona mwili wake una tattoo basi ujue kampeni yake na Motamma ya kuomba kuletewa mchora tattoo mjengoni ilifanikiwa.
Bongo Forest
BBA
Big Brother 'The Chase': Nando wa Tz amuomba Biggie amletee mtu wa kumchora Tattoo mjengoni

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment