Apparently watangazaji wengi wa kike wa clouds fm humchanganya sana Rapcellency Prezzo, Kama unakumbuka aliwahi kusema hasemi wala haongei kwa uzuri wa Dj Fetty.
Na sasa word on street ni kwamba jicho la rapper huyomwenye asili ya Kenya na Tz limetua kwa mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho, Diva Loveness Love. Wiki iliyopita Diva alimwalika Prezzo kwenye show yake na huenda ukaribu huo uliongezeka zaidi siku hiyo.
Kwa mujibu wa You Heard ya clouds fm, Diva na Prezzo ni item.
"Diva siwezi kumwachia bhana, nimwachie nichekwe", alisema Prezzo.
"Bado mahari tu mshkaji wangu inatoka kutoka mwanza, only time can tell. Nikikwambia sasa hivi ukweli ntamaliza uhondo, inaitwa yaani love at first sight, Diva mwenyewe umeshamuona she is classy yaani she is beautiful", alisisitiza Prezzo ambaye jina lake halisi ni Jackson Makini.
Hata hivyo Diva amekanusha kwa kudai kuwa yeye na Prezzo ni marafiki tu.
No comments:
Post a Comment