Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka
daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala
kuingia MTWARA
Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) Maaskari
wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake. Ni mapambano baina ya
vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi
limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
Gonga continue reading kuendelea..
Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
Matairi kila kona ya mji yamechomwa barabarani polisi na
zimamoto wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu
“Gesi haitoki hata kwa bomba la peni”
Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la
gesi. Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya
Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu
kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu
kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari
yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na
Lindi. Ving’ora vinalia ovyo ovyo.
watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia. Vituo vya Redio vya
Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine
vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea
maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake.
Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika.
Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.
Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia
ovyo. Kituo kimoja cha habari kinachorusha habari za bunge chazuia
mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na
kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye
wamerejesha matangazo yao)
Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe.
Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.
Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi
za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine
wanatembea na magari ya Serikali.
Maeneo yote yametawaliwa na ukimya. Kesho inaendelea tena kwa siku ya
pili. Serikali isipoangalia inaweza ikasababisha “Uprising” maeneo
mengine ya nchi.
No comments:
Post a Comment