Breaking News
recent

Unafahamu kwamba Jay-Z alihudhuria mechi ya Arsenal vs Man Utd...?

Hiphop star wa dunia, rapper Jay-Z alikua mmoja kati ya waliohudhuria mechi ya Arsenal vs Manchester United jana  zilitoka 1-1 ambapo pembeni yake, Jay Z alikua na mwimbaji ambae ni Lead singer wa Coldplay Chris Martin.

Hii ni mara nyingine tena kwa Jay Z kuhudhuria mechi ambayo Arsenal inacheza, aliwahi kuhudhuria ya Man City vs Arsenal kwenye uwanja wa Etihad mwaka 2010 akiwa mgeni aliealikwa na Man City ambapo baadae ripoti za waandishi zilisema Jay Z ni shabiki wa Man City.

Alipoongea na Jarida la Arsenal, J alisema… baada ya ile mechi naona kila mwandishi aliripoti kwamba mimi ni shabiki wa Man City, hapana…. kila mmoja U.K anajua kabisa kwamba mimi ni shabiki wa Arsenal”
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.