Breaking News
recent

Dotnata awekewa sumu kwenye Juice, yamwathiri Figo, Mbavu na Uti wa Mgongo

Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadaiwa kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.

Amesema alianza kuhisi kupandwa na presha ambapo alilazwakwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufika 284 huku wakimweleza huenda ni kwa kuwa amenenepa sana. Baadae alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.

Amesema tatizo hilo limesababisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.

"Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takribani mwezi wa nane (8) sasa, huyo mtu aliyenipa sumu alipitisha kwa njia ya juice".
Amesema Dotnata ambae kwa sasa ameokoka.

Akizungumza sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:-
"Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelee kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndo mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu".

Msikilize zaidi hapa:-

Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.