BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo
alikuwa akiliendesha aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine
kisha kumgonga mtembea kwa miguu.
Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema
alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo
barabarani.
Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi, hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi, hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na kutaka kumpiga vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu waliingilia kati na kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu wangemshushia kichapo.
“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.
No comments:
Post a Comment