Baada ya kusikia kupitia vyombo mbali mbali vya habari kuwa Mh mbunge
wa Kigoma Mjini Zitto ametangaza kuwania kiti cha uraisi ifikapo mwaka
2015, Zitto ameendelea kusisitiza msimamo wake kupitia mtandao wa jamii
wa Facebook
Narudia,
mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama
mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama
changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie
wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu
ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na
mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005
No comments:
Post a Comment