Rapper wa kundi la Rockers, Abbott Charles a.k.a Quick Rocker amesema ameanzisha record label yake aliyoipa jina la 255. Rapper huyo anaye tamba na club banger yake mpya iiywayo "katika" pia amefungua studi yake ya kurekodi inayoitwa "Big step"
Akiongea na kipindi cha Block 4teen cha DTV wiki iliyopita, Quick alidai kuwa studio yake inapatikana maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam. Hata hivyo hit maker huyo wa "Bullet" alisema pamoja na kuwa na studio yake mwenyewe bado ataendelea kufanya kazi na studio nyingine na kila aina ya producer ili mradi apate kitu kizuri.
Akiongelea wimbo wake mpya "katika" Quick Rocka alieleza kuwa aliamua kutoka tofauti kwa kuwa mziki wa Tanzania umebadilika ambapo watu wengi hupenda nyimbo zinazochezeka. Katika mahojiano hayo rapper huyo alizungumza pia uwezo wa kundi lake la "Rockers" ambalo limevunjika na kudai kuwa kundi hilo limerudi tena na mashabiki wategemee mambo mapya.

Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment