Breaking News
recent

Proscovia Alengot Oromait: Msichana mwenye miaka 19 aliyeshinda ubunge

Proscovia Alengot Oromait ameweka rekodi barani afrika kwa kuwa mbunge mwenye umri mdogo kulikowote kwa kuingia mjengoni akiwa na miaka19 tu. Kama ynadhani alipata kwa viti maalum, futa wazo hilo kwa sababu msichana huyo ameshinda kwenye uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge kilichokua kikikaliwa na baba yake.
Awali Oromait alipanga kwenda chuo lakini akajiingiza kwenye maswala ya siasa baada ya kifo cha baba yake Michael Oromait mwezi july, aliyekua mbunge wa jimbo la Usuk liliopo mashariki mwa Uganda. Akiwa na miaka hiyo Oromai aliwagalagaza wagombea watu wazima wanane ambapo alimzidi kura mara mbili mgombea aliyekua akimfuatia. Oromait amekuwa mbunge wa pili mwenye umri mdogo duniani.
Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.