
Sijawahi kuzungumza na mtu
akaniambia anahisi siku zake za kuendelea kuishi zimekaribia kuisha, sijawahi
kufanya mahojiano na mtu yeyote akaniambia amekata tamaa ya kuendelea kuishi
lakini staa wa muziki wa dance Banza Stone ndio amekua wa kwanza kunitamkia
hayo maneno.
Baada ya kukubali kwamba
amekata tamaa ya kuendelea kuishi, staa huyu ambae amepita kwenye bendi nyingi
za bongo ikiwemo African Stars (Twanga Pepeta), ameongea exclusive na
millardayo.com na kuthibitisha kwamba muda mfupi ujao ataingia studio kurekodi
nyimbo sita au 8 zitakazo elezea maisha yake, yani anataka hizo nyimbo ziwe
zinachezwa au kusikilizwa sana atakapofariki.
Namkariri akisema “ninavyovitarajia kwenda kuvirekodi kwenye hii album yangu mpya
miongoni mwa nyimbo hizi ‘ndivyo nilivyo’ na ‘maisha yangu’ zitawagusa watu
kiasi kwamba wanaweza wakatoa machozi”
Chanzo cha kufanya haya yote ni
kwasababu ameota ndoto siku chache zilizopita kwamba hana siku nyingi za kuishi
duniani, namkariri akisema “hiyo ndoto nimeiota siku mbili tatu, ndoto inaweza
kuwa na ukweli au isiwe kweli, najihisi kama nimekata tamaa kwenye maisha yangu
lakini nipo tayari Mungu akinipenda, mi siumwi isipokua nina imani kwamba ipo
siku tu Mungu akinipenda nitakwenda kwake siogopi kifo hata kidogo”
Kwenye line nyingine, Banza
amesema ni kweli sasa hivi anapitia kwenye maisha magumu kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kupungua kwa kipato chake.
No comments:
Post a Comment