President Jakaya Kikwete ambae pia ni
mwenyekiti wa CCM Taifa amewatoa wasiwasi wanachama wa CCM baada ya habari
kusambazwa kwamba chama hicho kinakaribia kumfia, yani kinafia mikononi mwake
kutokana na kushindwa kukiongoza.
Amesema wanaoeneza hayo maneno ni
wapinzani wa kisiasa ambapo amesisitiza kwamba uongozi wake hautasikiliza madai
hayo na utaendelea kupitisha viongozi kulingana na sifa zinazohitajika.
Kuhusu baadhi ya wagombea kukatwa majina
yao kwa madai ya upendeleo amesema hawajapitisha jina hata moja kama
ilivyopendekezwa na mikoa na badala yake wanawapitisha wagombea kulingana na
ujuzi, elimu na uzoefu ndani ya chama.
No comments:
Post a Comment