Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya KRC
Genk ya ligi kuu ya Belgium – Jupiter League – Mbwana Ally Samatta, jana
kupitia akaunti ya Instagram ameonyesha ‘ndinga’ yake aliyoinunua baada
ya kupata leseni ya kuendesha gari nchini Belgium.
Samatta ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kupata
majeruhi, jana usiku alikuwemo katika katika kikosi cha Genk
kilichoifunga Sassuolo 3-1 katika mchezo wa Europa League.
Gari alionunua Samatta ni Merecedez Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 –
ambayo imemgharimu kiasi cha €46,680 ambayo ukiizidisha kwa fedha za
madafu inakuwa zadi ya millioni 130.
Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment