Breaking News
recent

Hapa Kazi Tu: Said Fella Achimba Visima Vilivyokwama Kwa Miaka Mitatu Kwenye Kata ya Kilungule (Picha)

Kasi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kupiga kazi tu imewaambukiza viongozi wengine.
Muasisi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella ambae pia ni Diwani wa kata ya Kilungule ya wilaya ya Temeke Dar es Salaam ameanza kutekeleza ahadi zake.

Fella amekiambia chombo kimoja cha habari kuwa amenza kwa kuvirejesha visima vilivyoshindwa kutoa maji kwa miaka mitatu iliyopita.

Amesema wakati wa kampeni aliahidi kuwa angeanza kushughulikia kero ya maji kwenye kata yake ndani ya siku 30, ameongeza pamoja na visima, aliahidi pia kujenga kituo cha polisi kwenye kata hiyo pamoja na kutengeneza barabara. Chini ni picha za kazi hiyo.....


Mohamed Jaku

Mohamed Jaku

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.