Unaambiwa Zaidi ya daladala 1,800 hazitoruhusiwa kufanya safari zake
maeneo ya katikati ya jiji la Dar baada ya miundombinu ya mradi wa
mabasi yaendayo haraka kukamilika na ujenzi huo wa miundombinu hiyo
inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu ambapo mabasi 10 madogo na
makubwa 20 yatatoa huduma za awali kama majaribio.
Meneja wa uendeshaji wa Dar Peter Mnuo amesema huduma hii ya
majaribio inategemewa kutolewa December mwaka huu na huduma kamili
itaanza kutolewa kuanzia July 2015 ambapo wakala wa mabasi hayo yaendayo
haraka umekwishaanza maandalizi ya kutoa huduma ya awali ya mabasi
makubwa kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni ikiwa kama sehemu ya mfumo
wa kuanza kutoa huduma.
Mabasi hayo ya majaribio yanaweza kubeba jumla ya abiria 140 hadi 160
mpaka hapo itakapoanza kutolewa huduma kamili July 2015 ukiwa ni mradi
uliopangwa kutekelezwa kwa awamu 6 ambapo kwa awamu ya kwanza
unahudumiwa na fedha kutoka Benki ya dunia.
Mohamed Jaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment